Acha Dhamiri Yako Iwe Kielekezi Chako

Tuombeeni, maana tunaamini kwamba tuna dhamiri njema, tukitaka kuwa na mwendo mwema katika mambo yote (Waebrania 13:18)

Mungu hutupa dhamiri ili tukae mbali na mashaka. Tukipuuza dhamiri zetu kwa muda mrefu, hatutaweza tena kuhisi uthibitisho wa Mungu tukiwa tunahukumika kwa dhambi. Watu huja kuwa na mioyo migumu wanapopuuza hisi zao za kawaida za jema na baya. Hili hufanyika hata kwa watu waliozaliwa upya. Kadri wanavyokuwa na mioyo migumu, ndivyo inavyokuwa vigumu kwao kusikia sauti ya Mungu. Dhamiri zao hazitafanya kazi jinsi Mungu alivyopanga zifanye.

Dhamiri ni kazi ya roho na hufanya kazi kama msimamizi wa ndani wa tabia yetu. Hutufanya tujue iwapo kitu ni sawa au si sawa; hatimaye; maarifa yetu ya viwango na uelekezi ambao Mungu ametuwekea huathiri dhamiri zetu pakubwa.

Neno lake huamsha dhamiri kutoka hali ya kuzirai. Watu ambao si Wakristo huenda wakajua wanapofanya makosa, lakini huwa hawahisi uthibitisho kama wale waliozaliwa upya, kujazwa Roho Mtakatifu, na kushiriki na Mungu kila siku.

Kadri tunavyotumia muda wetu mwingi katika uwepo wa Mungu, ndivyo tunavyokuwa wahisivu zaidi kwa vitu ambavyo haviakisi moyo wa Mungu. Tunapoanza kuwa na tabia isiyokuwa ya kiungu, tunahisi mara moja kwamba tumeenda nje ya vile Yesu angetaka tushughulikie hali fulani.

Tunaweza kuwa na maisha ya ajabu tukijaza nia zetu kwa Neno la Mungu halafu tutii tu dhamiri zetu.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Acha dhamiri yako iwe kielekezi chako.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon