
Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamukuze Baba yenu aliye mbinguni. MATHAYO 5:16
Kabla hatujanunua kitu, tunapenda kuchunguza kiwango chake. Tunaponunua vitu, tunasoma vibandiko au tunatafuta alama fulani za biashara (majina ya rajamu) ambazo zina sifa ya kuwa na viwango vizuri vya ubora. Hilo ndilo ambalo watu wanafaa kufanya nasi kama wanafunzi wa Yesu. Upendo ndio alama ya biashara (ishara au sifa ya kipekee) ya Mkristo. Watu wanafaa kututambua sio tu kwa kile tunachosema, lakini kwa vile tulivyo pia.
Kama waaminio, tuna nafasi kubwa ya kuonyesha ulimwengu yule Yesu aliye. Tunafanya hivyo kwa kutembea katika upendo wake—upendo wa Baba uliofunuliwa na kuelezwa ndani ya Mwanawe na sasa unadhihirishwa ndani yetu. Neno linasema, “Acha nuru yako iangaze mbele ya watu,” na hakuna kinachoangaza zaidi kuliko upendo. Kumbuka kwamba una haki ya kumwakilisha Yesu kibinafsi, na ushukuru kwamba atakutumia kuwavuta watu kwake.
Sala ya Shukrani
Baba, asante kwa mfano ambao Yesu alitupatia wa jinsi ya kuwapenda wengine. Na asante kwa nafasi ya kumpenda kila mmoja ninayetangamana naye leo. Nisaidie kuangaza kwa nuru kuu katika ulimwengu wa giza.