Achilia, Acha na Usamehe

Achilia, Acha na Usamehe

Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu. —MARKO 11:25

“Achilia, acha na usamehe,” ni kile ambacho Biblia inasema tufanye na makosa (Marko 11:25). Ni muhimu kusamehe haraka. Tukifanya hivyo haraka, inakuwa rahisi zaidi. Gugu ambalo lina mizizi migumu ni migumu kung’oa kuliko ule ambao umeota tu muda mfupi uliopita.

Upendo hauhesabu mabaya; hautakabari, huvumilia, hauhusudu, hauoni uchungu (1Wakorintho 13:5). Tukijua haya, tunaweza kutazama maisha yetu binafsi na kuelewa kirahisi iwapo tunatembea kwa upendo. Iwapo una kitu moyoni dhidi ya mtu mwingine, fanya uamuzi mzuri sasa hivi “kuachilia, kuacha na kusamehe.”

Tuna nafasi nyingi sana za kuudhiwa, na kila wakati huwa tuna uteuzi wa kufanya. Tukichagua kuishi kwa hisia zetu, tutaendelea kuudhika na kufadhaika kila mara. Lakini tukichagua kuishi kwa upendo, tutawasamehe watu wakitukosea na kumtumainia Mungu kututetea, badala ya kuhisi kama ambao lazima tujitetee kila wakati.

Mungu ni upendo, na husamehe na kusahau: “Maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.” (Yeremia 31:34) Na anafurahia kufanya hivyo. Kadri tunavyomkaribia, ndivyo tunazidi kuwa kama yeye. Kwa usaidizi wa Mungu, tunaweza kujifunza kuishi maisha ya upendo na msamaha.


Unapoamua “kuachilia, kuacha na kusamehe,” furaha na ridhaa ndivyo matokeo ya kawaida.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon