Achilia Jivu

Achilia Jivu

Kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya jivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito… —ISAYA 61:3

Sehemu mojawapo ya mchakato wa urejesho katika maisha yetu ni kwamba Mungu hutupatia maua badala ya jivu. Lakini ili hilo lifanyike, lazima tuhiari kumpa jivu.

Huenda ulidhurika zamani na kuweka jivu la kudhurika mahali ambapo unaweza kulifikia. Kila wakati mmoja baada ya muda mrefu, huenda ukalichukua na kuomboleza juu yake tena. Iwapo ni hivyo, ninaelewa kwa sababu kuna wakati katika maisha yangu ambapo nilikuwa ninafanya vivyo hivyo.

Lakini ninataka kukuhimiza kufanya nilichofanya na uachilie jivu hilo, huku ukiruhusu upepo wa Roho Mtakatifu kulipeperusha hadi mahali ambapo haliwezi kupatikana tena. Hii ni siku mpya. Hakuna wakati zaidi uliopo wa kuomboleza juu ya jivu la zamani. Mstakabali wako hauna nafasi ya mambo yaliyopita.

Mungu ana mpango uleule mzuri juu ya maisha yako ambao alikuwa nao ulipowasili katika sayari hii. Hajawahi kubadilisha mawazo, na hatawahi. Kuanzia ule wakati tu ambao adui alikudhuru, Mungu amekuwa na wazo la kukurejesha moyoni mwake. Jua kwamba wewe ni wa thamani, wa kipekee, unayependwa na maalum machoni mwake. Ni wakati wa kwenda mbele!


Ruhusu Roho Mtakatifu kupeperusha jivu na kubadilisha jivu hilo na maua.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon