Achilia

Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu. —MHUBIRI 7:9

Kuna mambo fulani katika maisha ambayo una kiasi cha udhibiti juu yake—kwa mfano unaweza kudhibiti unayetumia muda wako naye, unachokula, na wakati wa kulala. Lakini na mambo mengine mengi usiyoweza kudhibiti, kama vile mambo ambayo husema juu yako au gurudumu lililoisha pumzi ukiwa katika shughuli zako. Vile unavyoshughulikia mambo usiyoweza kudhibiti—yawe makubwa au madogo—mara nyingi huamua kiwango cha mfadhaiko wako na ubora wa maisha na afya yako.

Nina mapendekezo mawili kuhusu kushughuIikia mambo usiyoweza kudhibiti. Kwanza, usipoweza kuyadhibiti, usiyawajibikie. Na pili, ninapenda kusema, “Fanya uwezayo, omba na uache Mungu afanye yaliyobaki.”

Mara nyingi watu wanaokasirika kuhusu mambo wasiyoweza kudhibiti huteseka kwa njia nyingi. Watu wanaoachilia huwa na maisha bora zaidi. Kuachilia mambo fulani hakumaanishi kwamba hujali; inamaanisha tu kwamba umekubali ukweli kwamba huwezi kufanya lolote kuyabadilisha wakati huo. Gurudumu limekwisha isha pumzi tayari. Kulibadilisha au kulirekebisha kwa utulivu kunaleta maana; kutupa hasira na kulipiga teke hakuleti maana. Tukishughulikia kila mfadhaiko unapotokea, hatutaishia kulipuka kwa mfadhaiko juu ya matuta tusioweza kuepuka katika barabara ya maisha.


Mungu anaweza hata kutumia jambo lisilofaa au masikitiko kwa wema wako. Yuko hapohapo nawe, na yuko usukani. Ukimwamini kushughulikia mambo, utaweza kuishi juu ya pandashuka za maisha kwa amani, furaha na nguvu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon