Aina Nzuri Kabisa ya Ujuzi

Aina Nzuri Kabisa ya Ujuzi

Maana naliazimu nisijue neno lolote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulubiwa. 1 WAKORINTHO 2:2 BIBLIA

Mtume Paulo alikuwa na ujuzi mwingi. Alikuwa mfarisayo wa mafarisayo, msomi, mwenye kuelimika. Na kabla ya kubadilishwa akiwa njiani kuelekea Damaski, alikionea fahari alichokijua. Si ni la ajabu kwamba kadri watu wanavyopata ujuzi ndivyo wanavyokuwa na majivuno?

Katika 1 Wakorintho 8:1, Paulo alisema kwamba ujuzi huleta majivuno. Tungejua kila kitu tunachofikiri tungependa kujua, tusingemwegemea Mungu kwa sababu tungekuwa na majivuno sana hata tukafikiri kuwa hatumhitaji.

Paulo alifanya mgeuko wa digrii-180 kutoka kwa kufikiria alijua kila kitu hadi kufikia kusema kuwa aliazimu asijue lolote ila tu Yesu Kristo naye amesulubiwa. Nafikiri Paulo alikuwa akisema, “Chote ninachokijua ni Yesu, na sina haja ya kujua kingine zaidi ya hicho.”
Yesu ndiye kitu muhimu zaidi. Fikiria kuhusu mfadhaiko ambao ungeepuka kwa kuacha wasiwasi na kujaribu kufikiria vile utafanya vitu na uamue kutojua chochote ila Yesu. Shukuru kuwa unaweza kufanya hivyo haswa!


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru, Baba, kwamba Yesu alikuja ulimwenguni humu na kufa kwa ajili ya dhambi zangu. Huenda nisiwe ninajua vile nitafanya kila kitu, lakini ninajua kitu kilicho muhimu zaidi: tumaini langu, amani, na furaha vyote vinapatikana katika upendo wako kwangu ambao umefunuliwa katika dhabihu ya Yesu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon