Amini na Upokee kutoka kwa Mungu

Amini na Upokee kutoka kwa Mungu

Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema. —YOHANA 1:16

Tena na Tena, Biblia husema kuhusu kupokea kutoka kwa Mungu. Humwaga kibali na baraka zake kila wakati. Ili kufurahia kibali hicho na baraka—na ili kuishi katika ushirika wa karibu na Mungu—ni muhimu tuchague kupokea bure vyote anavyotupatia.

Mojawapo ya changamoto zetu kubwa ni kwamba hatuamini neno bure. Tunatambua kwamba katika mifumo ya ulimwengu, vitu kwa kweli si vya bure. Hata kama tunaambiwa ni vya bure huwa kuna gharama iliyofichika mahali.

Lakini ufalme wa Mungu wa neema na upendo sio kama wa ulimwengu. Upendo wa Mungu wa ajabu ni kipawa anachotoa bure. Kile tunachohitaji kufanya ni kufungua mioyo yetu, kuamini Neno lake, na kulipokea kwa shukrani.

Haijalishi vile hali zinazokuzunguka zinavyoonekana leo, simama kwenye Neno la Mungu na utumainie kwamba wema wake na neema zinamwagwa juu ya maisha yako. Amini na uipokee leo.


Mfumo wa ulimwengu unasema, “Nitaamini nikishaona.” Ufalme wa Mungu unasema, “Nitaamini kabla ya kupokea.”

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon