Baba Yako Mtimilifu wa Mbinguni

Baba Yako Mtimilifu wa Mbinguni

Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao? MATHAYO 7:11

Iwapo mtu angekuwa na baba mwenye hasira, ni kawaida kumwona Baba Mungu kama aliye na hasira pia. Natumai wewe ni mmoja wa wale waliobarikiwa ambao walikuwa na baba mzuri wa dunia, lakini kwa wengi haikuwa hivyo.

Watoto ambao hukua na akina baba wenye hasira, wasiokuwepo au madhalimu mara nyingi huwa hawana hisia za usalama. Huwa wana hofu ya hukumu itakayotokea au hatari zinazoning’inia juu yao wakati wote. Lakini shukuru Mungu, Baba yako wa mbinguni ni tofauti na akina baba wote wa dunia. Iwapo baba yako hakuwepo, jua kwamba Mungu hatawahi kukuacha. Iwapo baba yako alikuwa mdhalimu au mwenye hasira, Baba yako wa mbinguni anataka kukupa thawabu maradufu kufidia mashaka ya awali (tazama Isaya 61:7).

Haijalishi vile baba yako alikosa kuwa mwaminifu kwako, ninakusihi tu usiruhusu hilo liharibu maisha yako. Fanya uamuzi wa kuamini ukweli kwamba Baba yako wa mbinguni ni mwaminifu na anakupenda sana.


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwamba ninaweza kukutazamia kuwa mzazi ambaye sikuwa naye. Nisaidie kusamehe dhuluma nilizovumilia nikiwa mtoto, na kusonga mbele nawe kwenye maisha mapya, yenye furaha na amani. Ninashukuru kwamba wewe ni Baba wa mbinguni uliye mtimilifu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon