Kamba zangu zimeaniangukia mahali pema, naam nimepata urithi mzuri. ZABURI 16:6
Umewahi kusita ili kufikiria kuhusu vile vitu unafaa kushukuru kwavyo?
Ukiamka asubuhi hii na sehemu nyingi za mwili ambazo hazina maumivu kuliko zile ambazo zina maumivu, umebarikiwa. Iwapo una chakula, mavazi, na mahali pa kukaa, uko salama kuliko zaidi ya asilimia 75 ya ulimwengu. Iwapo una pesa benkini, mkobani mwako, au salio la pesa nyumbani, wewe ni miongoni mwa asilimia 8 ya watu matajiri ulimwenguni. Kama hujawahi kupitia hatari za vita, upweke wa jela, uchungu wa mateso, au njaa uko mbele ya watu milioni 500 ulimwenguni. Ukisoma ujumbe huu, umebarikiwa zaidi kuliko watu bilioni mbili ulimwenguni wasioweza kusoma.
Usipuuze baraka yoyote—shukuru Mungu kila siku kwa wema wake katika maisha yako.
Sala ya Shukrani
Baba, nisaidie kutambua vile nimebarikiwa. Asante kwa afya yangu, nyumbani kwangu, familia yangu, faida nilizopewa, na hewa ninayovuta. Ninachagua kufikiria kuhusu kile nilicho nacho badala ya kile ambacho sina. Asante kwa maisha yangu ya ajabu.