Bora Kuliko Kujiamini

Bora Kuliko Kujiamini

Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. —WAFILIPI 4:13

Hakika kijumla hurejelewa kama “Kujiamini” kwa sababu tunajua sisi sote kwamba tunahitaji kuhisi vizuri kujihusu iwapo tutatimiza kitu chochote maishani. Tumefundishwa kwamba watu wote wana hitaji la kimsingi la kujiamini. Ingawaje huo sio ukweli mkamilifu.

Zaidi ya kujiamini—tunahitaji kumwamini Yesu ndani yetu. Hatuwezi kujifikiria tuko juu tukiwa kando naye. Tunaweza kufanya mambo ya ajabu lakini kupitia kwa Yesu tu!

Tukiamini uongo wa “kujiamini,” tutaanzisha matatizo mengi ya kutatanisha. Tutaishi katika hofu na kukosa usalama, na tutaridhika na machache kuliko uwezo wetu mkamilifu ndani ya Kristo.

Usijijali, udhaifu wako, au nguvu zako. Mtazame Mungu. Iwapo wewe ni dhaifu, anaweza kukutia nguvu. Iwapo una nguvu zozote ni kwa sababu alikupa. Kwa njia yoyote ile mtazame Mungu na utie hakika yako ndani yake.


Hatuhitaji hakika ya kibinafsi; tunahitaji hakika ya Mungu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon