Chanzo cha Kweli cha Tumaini

Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili. —WAFILIPI 3:3

Ufunguo muhimu wa kuwa na nguvu kiroho na salama zaidi ni kugundua chanzo cha kweli cha tumaini.

Unatia tumaini lako katika kitu gani leo? Je, katika kiwango chako cha elimu, kundi lako la kijamii, kiwango cha pesa ulicho nacho, au nafasi uliyo nayo kazini—au lina shina ndani ya Mungu? Hilo swali linafaa kujibiwa na kila aaminiye anayetamani kumkaribia Mungu kila siku.

Tukiweka tumaini letu lote ndani ya elimu yetu, sura zetu, hadhi zetu, vipawa vyetu, talanta zetu, au katika maoni ya watu wengine, tutaishia kusikitika na kuwa na dhiki kwa sababu ya kukosa usalama. Baba yetu wa mbinguni anatuambia, “Hata ingawa huenda watu na vitu vikakufeli, mimi sitawahi. Unaweza kuweka imani na tumaini lako ndani yangu.”

Ninakuhimiza kuja mahali ambapo tumaini lako halitakuwa katika mwili au vitu vya huu ulimwengu, lakini ndani ya Yesu Kristo. Ni yeye pekee atakayekutia nguvu, atasimama nawe kila wakati, na hatakufeli.


Kwa uaminifu, chunguza tumaini lako liko ndani ya kitu gani, na iwapo liko katika chochote kando ya Mungu, tubu (badilisha mawazo yako kwa wema), na uwe tayari kufanya vitu kwa utofauti.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon