Chukua Wakati Kujua Mungu

Basi msihukumu hukumu ya macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki (YOHANA 7:24)

Andiko la leo ni neno maalumu lililo wazi kutoka kwa Mungu hadi kwetu sisi. Anatukanya kufanya hukumu ya juujuu au ya macho.

Kwa muda wa miaka mingi, nilikuwa aina ya mtu ambaye alifanya hukumu za haraka. Mungu alinishughulikia kuhusu hilo mara nyingi, na mwishowe nikatambua hatari ya kutoa hukumu ya haraka na ya macho.

Kabla tuhukumu watu, tunafaa kuchukua muda kujua wao ni nani kwa kweli. Ama, (1) tunaweza kumkubali mtu kwa sababu wanaonekana kuwa kitu, ikiwa kweli si kitu; au (2) tunaweza kutomkubali mtu kwa sababu ya jinsi anavyoonekana nje au kitendo alichofanya, na kumbe huyo mtu ni mzuri sana ndani kwa kweli.

Sisi wote tuna tabia zetu fulani za pekee, matendo yetu madogo yasiyo ya kawaida, tabia na njia zisizoeleweka na wengine. Mungu mwenyewe hahukumu kwa macho na tunahitaji kufuata mfano wake.

Daudi asingechaguliwa kuwa mfalme iwapo watu wangehukumu kwa macho. Hata familia yake yenyewe ilimpuuza. Lakini Mungu aliuona moyo wa Daudi, moyo wa mchungaji. Mungu aliona mwabudu, mtu aliyekuwa na moyo wake, mtu ambaye aliweza kupinduliwa na kufinyangwa katika mkono wake. Hizi ndizo sifa ambazo Mungu huthamini, lakini huwa hazionekani tu kwa kupiga macho.

Ninakuhimiza kutafuta Mungu na kuruhusu Roho Mtakatifu kukuzungumzia kuhusu watu. Anajua mioyo yao, na atakuambia iwapo utajihadhari na uhusaino fulani au utaendelea nao. Mwamini, usiamini hukumu yako, kukuongoza unapoendelea kujua watu na kukuza mahusiano.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Kuwa na nia ambayo ungependa wengine wawe nayo kwako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon