Dhamira Ya Imani

Dhamira ya Imani

. . . Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yaleyale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani. —1 Petro 5:8–9

Mara nyingi huwa tunafanya makosa ya kujaribu kutumia imani kupata kufikia mahali palipo na uhuru kutokana na mashaka. Lakini sio tu kila mara ambapo dhamira ya imani hutuzuia kupata mashaka; inadhamiria kutupitisha katika mashaka. Kama tusingekuwa na mashaka, tusingehitaji imani yoyote.

Majaribu ya kutoroka shida zetu yapo, lakini Bwana anasema lazima tuyapitie. Habari njema ni kwamba ameahidi kwamba haitalazimu tupitie peke yetu. Atakuwa hapo kila mara kutusaidia katika kila njia. Ametuambia, “Usiogope, kwa kuwa niko nawe” (Isaya 41:10).

Katika maisha yetu ya kila siku, tunaweza kujifunza kusimama imara na kupinga shetani. Kujifunza kutoyumbayumba katika nyakati ngumu ni mojawapo ya njia nzuri za kusonga karibu na Mungu na kupitia katika ugumu wowote ambao huenda tukakumbana nao. Mungu yuko nawe kukusaidia, kwa hivyo usikate tamaa!


Shetani atakata tamaa akiona kwamba hutavunjika moyo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon