Dhamiria Uwezo, sio Udhaifu

Dhamiria Uwezo, sio Udhaifu

Basi kwa kuwa tuna karama, zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa… —WARUMI 12:6

Kuamini uwezo ambao Mungu ameweka ndani yako ni sehemu muhimu ya kujenga ujasiri na kushinda kutokuwa na usalama. Unapodhamiria kutazama uwezo wako badala ya udhaifu wako, unampa Mungu nafasi ya kufanya kazi, kwa sababu unaamini kwamba ana mpango juu ya maisha yako.

Ingawa huenda watu wakasema, “Unaweza kufanya chochote ambacho umedhamiria kufanya,” kwa kweli mimi na wewe hatuwezi kufanya chochote… katika nguvu zetu. Na hatuwezi kufanya chochote au kila kitu ambacho tunaona watu wengine wakifanya. Lakini tunaweza kufanya kila kitu ambacho Mungu ametuita kufanya. Na tunaweza kuwa chochote ambacho Mungu anasema tunaweza kuwa.

Kila mmoja wetu amejaa vipawa na talanta, nguvu na uwezo. Kusema kweli tukianza kushirikiana na Mungu, kutambua nguvu zetu na kuridhika na kile ambacho ametupatia, tutatambua uwezo wetu mkamilifu. Vipawa na talanta hutolewa na Roho Mtakatifu kulingana na neema iliyopewa kila mmoja kuvitumikisha.

Iwapo utainuka katika maisha, iwapo utavitumikisha zaidi vile vitu ambavyo Mungu amekupa, dhamiria kutazama uwezo wako—kile ambacho Mungu amekuumba kuwa—sio kwa udhaifu wako.


Iwapo Mungu amekuita kufanya kitu, utajipata ukikipenda hata kama huenda unakabiliana na matatizo gani.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon