Elekeza Nia yako na Udumishe Mwelekeo wake

Elekeza Nia yako na Udumishe Mwelekeo wake

Yafikirini yaliyo juu, na udumishe fikra kwa vitu vilivyo juu siyo yaliyo katika nchi. —WAKOLOSAI 3:2

Tunaweza kuwa na mkao mzuri au mbaya wa nia. Ule mzuri hutufaidi, na ule mbaya hutudhuru na kuzuia kuendelea kwetu. Kwa usaidizi wa Mungu, tunaweza kuelekeza nia zetu katika sehemu inayofaa.

Watu wengine wana mtazamo hasi wa maisha kwa sababu wamepitia katika hali za mashaka katika maishani mwao mwote na hawawezi kufikiria lolote zuri. Halafu kuna watu wengine wanaoona kila kitu kama hasi kwa sababu tu nafsi yao inaegemea upande huo. Haijalishi sababu yake mwono hasi humwacha mtu taabani na uwezekano wa kutokua kiroho. Ili kufurahia mpango mwema wa Mungu juu yetu, tunahitaji kukubaliana naye, na bila shaka hana uhasi!

Kwa usaidizi wa Mungu na bidii yako na ukakamavu, unaweza kuvunja mkao hasi wa nia na tabia za kale ambazo zinajaribu kukuweka mbali na Mungu. Shetani hataki upenye kwa sababu anajua kwamba ukifanikiwa, utafurahia maisha yako na kuwa baraka kwa wengine.

Maisha yako yatabadilika, jambo ambalo litasababisha maisha mengine mengi kubadilika. Ukielekeza nia yako upande unaofaa, itakuleta karibu na Mungu na kukuruhusu kutimiza kusudi lako ulilopangiwa na Mungu.

Tarajia mambo mazuri kufanyika kwako na kupitia kwako!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon