
Bwana akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili. Hesabu 6:25
Unapoendelea na shughuli zako za siku, mwombe Bwana akuangazie nuru za uso wake. Mwombe akuinulie uso wake na kukupa amani. Mwombe akuangazie utukufu wake, vile alivyomwangazia Musa. Halafu uache nuru hiyo iangaze mbele ya watu, wapate kuiona na kumtukuza Baba yenu aliye mbinguni (tazama Mathayo 5:16 Biblia).
Kuacha nuru yako kuangaza inaweza kuwa rahisi kama kuweka tabasamu kwenye uso wako. Jizoeshe kuwatabasamia watu na utawapata wengi wao wakifanya vivyo hivyo. Nuru ya utukufu wa Mungu imo ndani yako, lakini kama huwa huionyeshi nje, watu hawatabarikiwa. Ni ajabu litakalofanyika iwapo tu utashukuru, utabasamu na uwe mzuri kwa watu. Onyesha kibali kila mara uwezavyo kwa wengi uwezavyo. Kwa kufanya hiyvo, utapokea kibali, kwa sababu tumeambiwa kwamba chochote tunachopanda, ndicho tutakachovuna (tazama Wagalatia 6:7).
Sala ya Shukrani
Ninakushukuru, Baba, kwa nafasi ya kuwa nuru katika ulimwengu wa giza. Acha nuru na uzima wako uwangaze ndani yangu ili wengine waone. Ninashukuru kwamba kwa usaidizi wako, maisha yangu yanaweza kuwa baraka kwa wengine.