Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. YOHANA MTAKATIFU 16:33
Amani ni mojawapo ya baraka kuu ambayo Mungu ametupatia, na tunafaa kumshukuru kwa sababu ya hilo kila siku. Kutamani tu maisha ya amani haitoshi. Lazima utafute kuwa na amani na Mungu, amani na wewe mwenyewe, na amani na walio karibu nawe. Nimepata kwamba kadri ninavyojawa na shukrani, ndivyo ninavyokuwa na amani zaidi. Shukrani hunisaidia kuona nilicho nacho badala ya kile sina, hivyo kuniruhusu kuona baraka zangu badala ya kuwa na wasiwasi.
Kutembea kwa amani kukiwa muhimu kwako, utatia bidii inayohitajika ili uwe nayo. Nilitumia miaka mingi kuomba Mungu kunipa amani na mwishowe nikagundua kuwa alikuwa tayari ashatupatia amani, lakini ililazimu niichague. Yesu alisema katika Yohana 14:27, “Amani nawaachieni.” Tayari Yesu amekupa amani yako. Amua kutembea katika amani hiyo leo!
Sala ya Shukrani
Baba, asante kwamba umenipatia kila kitu ninachohitaji ili kuishi kwa amani. Leo, ninachagua kushikilia amani hiyo na kuishi kwa utulivu, huku nikijua kuwa wewe ni mkubwa kuliko majaribu au matatizo yoyote ambayo huenda ninapitia. Wewe ni kila kitu ninachohitaji. Wewe ni amani yangu.