Fanya Maisha yawe ya Kupendeza

Fanya Maisha yawe ya Kupendeza

Lolote lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana wala si kwa wanadamu. —WAKOLOSAI 3:23

Maisha hayakukusudiwa kuwa kuchosha na kutopendeza. Hatukuumbwa tu na Mungu kufanya kitu kilekile tena na tena hadi kikose maana kabisa. Mungu ni mbunifu. Iwapo hufikirii hivyo hebu tazama ulipo. Wingi wa wanyama, wadudu, miti, ndege na viumbe vingine vilivyo na uhai ni vya kipekee, si vya kawaida, na ni vya ajabu mno.

Uliumbwa kuwa wa kipekee, si wa kawaida, na wa ajabu kabisa pia. Ndiyo maana ninafikiria ni vizuri mara moja moja kufanya kitu ambacho kwa watu kitaonekana kuwa si cha kawaida na pengine hata kwako. Fanya kitu ambacho watu hawatatarajia. Itafanya maisha yako yapendeze na kuzuia watu wengine kufikiri wamekuweka vizuri katika vijisanduku vyao vidogo walivyotengeneza wao.

Mwanamke mmoja aliyekuwa na umri wa miaka sabini na sita alisema kwamba lengo lake kila wiki lilikuwa kufanya kitu kimoja kisichokuwa cha kawaida. Si hilo ni wazo zuri? Ukifanya kitu kisicho cha kawaida kimaksudi kila siku, hii itakuzuia kukwama, kuchoka na kutokuwa na shauku kuhusu maisha yako.

Utafanya kitu gani kisicho cha kawaida leo?


Kataa kuchoka na kuishi kwa kujikokota. Kuwa mbunifu na uongeze raha kwa chochote unachofanya.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon