fuata miongozo midogo

fuata miongozo midogo

na masikio yako yatasikia neno nyuma yako, likisema, Njia ni hii, ifuateni; mgeukapo kwenda mkono wa kulia, na mgeukapo kwenda mkono wa kushoto. Isaya 30:21

 Roho Mtakatifu daima anataka kutuongoza kwa njia ya uzima, lakini wakati mwingine tunajihusisha na masuala yanayoonekana kama “makubwa” hadi hatutambui kiasi gani anachosema nasi kwa njia ndogo ndogo kila siku.

Nilikuwa njiani nyumbani siku moja na nia ya kusimama na kupata kikombe cha kahawa, wakati huo nikawa na hisia kali kwamba ni lazima nimuite msaidizi wangu na kumwuliza ikiwa anataka kikombe pia. Nilipomwita, akasema, “Nilisimama hapa nikadhani, ningependa kikombe nzuri cha kahawa hivi sasa.” Unaona, Mungu alitaka kumpa tamaa ya moyo wake, naye alitaka kufanya kazi kupitia mimi. Sikusikia sauti kubwa au kuona malaika au kuwa na maono. Nilikuwa na hisia ya ndani au mawazo kwamba ni lazima nimpe kikombe cha kahawa. Kwa njia hiyo hiyo, Mungu anataka kuwabariki watu katika maisha yako. Ninakuhimiza leo kuweka moyo wako uisikie sauti ya Mungu. Fuata miongozo mdogo. Atasema kwa moyo wako na kukuongoza katika njia unayopaswa kwenda.

 OMBI LA KUANZA SIKU

 Roho Mtakatifu, leo nachagua kujituliza ili nisikie sauti yako ndogo. Nionyeshe njia ambazo ninaweza kuwabariki wengine.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon