Fungua moyo wako wa huruma

Fungua moyo wako wa huruma

Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.  1 Yohana 3:17-18

Kama Wakristo, Mungu huweka huruma ndani ya kila mmoja wetu, lakini ni juu yetu kuamua kama tutaufunga au kufungua moyo wetu kuupata. Nimeona kwamba jambo moja ambalo linaweka moyo wangu wa huruma wazi ni kufikiria kwa kiasi kikubwa juu ya mahitaji yaliyo katika dunia leo. Tunahitaji kugeuza mawazo yetu kwa wale walio na shida zaidi kuliko sisi na kufungua mioyo yetu kwa wale wanaosumbuliwa.

Soma 1 Yohana 3: 17-18. Ninayapenda maandiko haya kwa sababu yanasisitiza hasa kusema kwamba wakati ninapoona haja, siwezi kuipuuza tu kama wajibu wa mtu mwingine. Wala siwezi kufikiri kwamba haja ni kubwa sana, siwezi kufanya chochote juu yake, ambayo si kweli. Nimegundua katika huduma yetu kwamba hata kama wewe na mimi hatuwezi kufanya kila kitu kuhusu hali, tunaweza kufanya kitu. Na kitu ambacho tunaweza kufanya ni kuleta tumaini kwa watu.

Naomba uruhusu moyo wako wa huruma ufunguliwe wazi kwa mahitaji ya watu duniani kote.

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, sitaki kuishi kwa ubinafsi bila kujali mahitaji ya wengine. Mimi naufungua moyo wangu kupokea huruma yako ili niweze kuwasaidia wengine.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon