Funguo Nne za Mafanikio

Funguo Nne za Mafanikio

Naye Daudi akatenda kwa busara katika njia zake zote naye Bwana alikuwa pamoja naye. 1 SAMWELI 18:14

Katika kila unalojaribu kufanya, kuna funguo nne za mafanikio. Iwapo hizi tabia zitakuwa sehemu mojawapo ya kaida za maisha yako, zitakuwezesha kusonga kwenye mafanikio unayoyatamani.

  • Kujitolea: Bila kujitolea, watu hukata tamaa kwa urahisi; huwa hawana nguvu za kuendelea kabisa.
  • Kudhamiria: Kudhamiria hutuwezesha kufikia malengo na kufuatilia ndoto ambazo zinaonekana kutowezekana.
  • Kumngoja Bwana: Mafanikio yanapokosa kuja kwa urahisi, tunahitaji kumngoja Bwana na kupata nguvu zetu ndani yake.
  • Kuburudishwa na Kugeuzwa: Sisi wote huhitaji wakati mrefu wa urejesho na ugeuzwaji ili tujitayarishie changamoto mpya zilizo mbele.

Chunguza maisha yako mwenyewe na ujiulize iwapo unahitaji kuboreka katika eneo lolote na ushukuru kuwa huhitaji kufanya vitu hivi peke yako. Mungu yuko nawe na, unapomtafuta, atakupa kujitolea, kudhamiria, na uwezo wa kumngoja, na ugeuzwaji unaohitaji ili kufanikiwa.


Sala ya Shukrani

Baba, ninapokabiliwa na hali ambapo mafanikio yanaonekana kutowezekana, nisaidie kukumbuka kukuomba nguvu. Ninakushukuru kwamba utaniwezesha kufanya yote niwezayo ili kuishi maisha bora.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon