
Ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo. WAKOLOSAI 1:28 BIBLIA
Uhusiano wako na Mungu unapokomaa, utajipata ukiishi bila miongozo, kanuni na kaida na badala yake utaishi zaidi kwa matamanio ya moyo wako. Unapojifunza Neno zaidi, utapata matamanio yake yakiujaza moyo wako kwa shukrani na furaha. Mungu anataka uujue moyo wake kiasi cha kwamba utataka kufuata kichocheo, uongozi, na mwelekeo wa Roho Mtakatifu.
Mara tu unapokuwa huru ndani ya Yesu, simama ndani ya uhuru huo na usinaswe tena chini ya kongwa la utumwa (tazama Wagalatia 5:1). Mungu anataka kukuleta mahali papya palipojaa uhuru, kwa hivyo fuata moyo wako, kwa sababu hapo ndipo amri yake ilipo.
Sala ya Shukrani
Asante, Baba, kwamba kadri ninapotumia muda zaidi katika Neno lako, ndivyo ninavyolipenda zaidi. Ninaomba kuwa Neno lako litaujaza moyo wangu ili matamanio yangu yaanze kulingana na maagizo yako na mwelekeo wa maisha yangu. Asante kwa kuwa unanikomaza ndani yako.