Furahia katika tumaini la kupata kibali cha Mungu

Furahia katika tumaini la kupata kibali cha Mungu

Ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu. Warumi 5:2

Biblia imejaa ahadi za matumaini kwako na mimi. Tuna uwezo wa kuufikia uwepo wa Mungu. Anataka kutuponya magonjwa yetu. Atakutana na mahitaji yetu yote. Kuna mengi zaidi … mengi sana kuhesabu! Ndio maana ni ya kusikitisha sana wakati Wakristo wanapoteza ahadi za Mungu kutokana na ukosefu wa imani.

Hapa kuna swali: Je! Unatarajia ahadi hizo? Mambo mazuri yanaanza kutokea wakati unapofurahia matumaini ya kupata kibali cha Mungu mara kwa mara.

Luka 2:52 inatuambia kwamba Yesu aliongezeka katika … kibali na Mungu na mwanadamu. Wewe na mimi tunapata kibali cha Mungu kwa imani. Tunaweza kuongezeka katika kibali hicho na kupata ahadi zake kama Yesu. Na hata kama huoni vitu hivi katika maisha yako sasa, unaweza kufurahi na kuweka matumaini yako kwa Mungu, ukijua kwamba vitakuja.

Kila kitu kilichoahidiwa katika Biblia ni kwetu. Kwa hiyo furahia katika tumaini la kupata utukufu wa Mungu hivi sasa na atafanya mambo ya ajabu kutokea katika maisha yako.

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, natarajia na kufurahia ahadi zako kwa ajili yangu. Ninaamini kwamba Unaweza kuleta kila kitu ambacho nimeahidiwa katika Neno lako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon