Furahia Matunda ya Kazi Yako

Furahia Matunda ya Kazi Yako

Mwanadamu hapati jema kupita kula na kunywa, na kuiburudisha roho yake kwa mema katika kazi yake. Hayo nayo naliona ya kwamba hutoka mkononi mwa Mungu. MHUBIRI 2:24

Si mpango wa Mungu kwamba wanawe wasifurahie kazi ya mikono yao. Ni vizuri kufanya kazi kwa bidii, lakini ni vizuri pia kutenga muda ili kufurahia maisha. Shukuru kwamba Mungu ni Elishadai, Mungu wa zaidi ya vyote. Ni Yehova Jire, Bwana Mpaji wetu. Alisema kwamba anaweza kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu (tazama Waefeso 3:20).

Bila shaka Mungu anataka na hata anatuamuru kutumikia na kuwapa watu wengine vitu kwa ukarimu—lakini Mungu hakukusudia tuhisi kuhukumika tukitenga muda kufurahia matunda ya kazi yetu. Bidii ya kazi inastahili kutuzwa, na tusiwahi kufikiria kuwa haituzwi. Mungu huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii (tazama Waebrania 11:6), Kwa hivyo tenga wakati wa kutulia na kufurahia vitu ambavyo amekutuza navyo.


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwamba ninaweza kufurahia matunda ya kazi yangu. Nisaidie kupata kiasi kati ya kufanya kazi kwa bidii na kufurahia nilichofanyia kazi. Nisaidie kufurahia kile ulinipa nguvu ili kufanya kazi kukipata.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon