Furahia Thawabu

Furahia Thawabu

Na mwanadamu atasema, hakika iko thawabu yake mwenye haki. Hakika yuko Mungu anayehukumu katika dunia. ZABURI 58:11

Kutenga muda kufurahia tunda la kazi yako ni mojawapo ya vitu muhimu ambavyo vitakufanya ukaze mwendo katika nyakati ngumu.

Mungu aliwapa wanaume na wanawake wengi katika Biblia kazi ngumu ili wafanye, lakini alikuwa akiahidi thawabu kila wakati. Kutazamia thawabu hutusaidia kuvumilia matatizo. Biblia inasema katika Waebrania 12:2 kwamba kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuumeni wa kiti cha enzi cha Mungu.

Ninakuhimiza kutoangalia tu kazi unayofanya, lakini angalia pia ahadi ya thawabu. Chukua muda wa kushukuru na kufurahia tunda la kazi yako halafu utatiwa nguvu ya kumaliza safari yako.


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwamba ninaweza kutarajia thawabu yako kila wakati katika maisha yangu. Ninashukuru kwamba nyakati ngumu hazidumu milele, lakini ninaweza kujifunza kutokana na nyakati kama hizo na kutarajia wema wako katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon