Utanijulisha njia ya uzima; mbele za uso wako ziko furaha tele ; na katika mkono wako wa kuume mna mema ya milele (ZABURI 16:11)
Ninapenda kulala kifudifudi sakafuni ninapoomba- nikizungumza na Mungu na kusikiliza sauti yake. Huu mkao hunisaidia kufungia kila kitu nje na kuhisi kama ambaye niko peke yangu na Mungu. Niliomba hivyo hadi mkao huo ulipoanza kuumiza mgongo wangu na nikaacha! Ninafurahi kwamba sikuhisi kuwa mimi si wa kiroho kwa sababu ya kubadilisha mkao wangu wakati wa maombi. Ninachoweza kukuambia ni kwamba hakuna mkao ambao lazima ung’ang’anie kudumisha ili uombe, kuhisi uwepo wa Mungu, au kusikia sauti yake. Magoti yako yakiumia, lala sakafuni. Mgongo wako ukiumia, au uanze kulala ukiwa sakafuni, amka utembeetembee. Ukiwa wewe ni kama Dave anayeomba akiwa ameketi na kuangalia nje ya dirisha, basi vuta kiti chako. Tafuta mahali palipo patulivu na njia ambayo utazungumza na kumsikiza Mungu bila fujo wala kukatizwa.
Kuwa huru kutokana na vitu vyote ulivyosikia kuhusu fomula za maombi au mikao ya maombi- na uombe tu! Ninakutia changamoto ya kurahisisha mawasiliano yako na Mungu. Zungumza naye na umsikilize kwa njia ambazo ni tulivu na rahisi kwako- na zaidi ya yote, Furahia uwepo wake!
NENO LA MUNGU KWAKO LEO:
Omba tu!