Haja Muhimu

Haja Muhimu

Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, maana kwa matunda yake mti hutambulikana. —MATHAYO 12:33

Kwa aaminiye, fikra nzuri ni kitu muhimu sana kiasi kwamba mtu hawezi kuishi bila—kama vile mpigo wa moyo ulivyo muhimu na mshinikizo wa damu ulivyo muhimu. Kuna vitu ambavyo bila kuwepo, maisha yanakoma. Chanzo cha maisha yetu, chanzo cha mawazo yetu mazuri, ni ushirika wa mara kwa mara na Mungu katika Neno na maombi.

Biblia inasema kwamba, mti hujulikana kwa matunda yake. Hilo ni kweli kuhusu maisha yetu. Fikra huzaa matunda. Waza mawazo mazuri na matunda yatakayokuwa katika maisha yako yatakuwa mazuri. Waza mawazo mabaya, na matunda yatakayokuwa katika maisha yako yatakuwa mabaya.

Kwa kweli unaweza kuangalia mielekeo ya mtu na kujua aina ya mawazo ambayo hujitokeza katika maisha yake. Mtu mzuri mwenye huruma hana fikra za kutosamehe. Kwa upande ule mwingine, mtu mwovu hana mawazo mazuri yanayopendeza.

Unapopitia siku yako leo, ninakuhimiza kuwaza mawazo chanya mazuri ya kiungu na uyaruhusu kuanzisha mkondo wa maisha yako, maana mtu ajionavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo (Mithali 23:7).

Kadri unavyochukua muda kusoma Neno la Mungu, ndivyo itakuwa rahisi kukataa mawazo mabaya na kuchagua mawazo mazuri.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon