Hakuna Visababu

Hakuna Visababu

Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema Bwana. —YEREMIA 1:8

Hata iwe ni changamoto, kizuizi, au nafasi, tukijua Mungu yuko nasi, tunaweza kukabiliana na vitu vilivyo mbele yetu. Kutoroka si uteuzi mzuri. Chochote unachotoroka kitakuwa kinakungoja mahali pengine. Nguvu zetu za kushinda zinapatikana katika katika kuishi karibu na Mungu na kuchuchumilia mbele naye.

Yeremia alikuwa mwanamume mdogo sana ambaye alipewa kazi kubwa sana. Mungu alimwambia kwamba alikuwa ameitwa kama nabii wa mataifa. Alikuwa awe kipaza sauti cha Mungu. Wazo hilo lilimwogopesha Yeremia, na akaanza kuwa na visababu vingi kuhusu ni kwa nini asingeweza kufanya kile Mungu alikuwa anataka afanye.

Yeremia alikuwa anafanya makosa ya kwanza ambayo mimi na wewe huwa tunafanya—alikuwa anajitazama pamoja na uwezo wake. Kile Yeremia alihitajiwa kufanya ni kumtazama Mungu. Alikuwa akiwatazama watu akishangaa vile watakavyofikiria na kufanya iwapo angechukua hatua ya ujasiri ambayo Mungu alikuwa akimhimiza kuchukua. Mungu alimwambia Yeremia kukumbuka tu kwamba alikuwa naye na hilo ndilo Yeremia alihitaji.

Katika msitari wa mwisho wa sura ya kwanza, Bwana alimwambia Yeremia kwamba watu watampinga, lakini hawatashinda kwa sababu moja rahisi: “Niko nawe.”

Chochote unachokabiliana nacho leo, jipe moyo. Mungu anakabiliana nacho nawe.


Unapotoa macho yako kwenye hali zako, na uyaweke juu ya Mungu, una hakika ya kushinda.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon