Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. MATHAYO 11:28
Kwa kweli tunaishi katika ulimwengu ambao muda umekuwa mchache; kila kitu tunachofanya huonekana kuwa cha dharura. Tunaishi chini ya mshinikizo mkuu na kukimbia hapa na pale kutoka kwa kitu kimoja hadi kingine—kiasi kwamba huenda tukakosa kutekeleza vitu ambavyo ni muhimu sana katika maisha: familia, afya yetu, Mungu, na kujenga maisha yetu ya kiroho.
Ukweli ni kwamba hatuwezi kupambana na maisha bila Mungu. Hatuwezi kupambana na huo mshinikizo, kuchanganyikiwa huko, na mfadhaiko bila yeye. Ndoa zetu zitasumbuka, tutakuwa na mshinikizo wa kifedha, na mahusiano yetu hayatanawiri tusiposoma Neno la Mungu na kutenga muda kuomba.
Lakini kuna habari njema zinazotupa sababu ya kushukuru—Mungu atatutia nguvu na kutuwezesha kukabiliana na maisha kwa amani na hekima iwapo tutaanza kuomba kuhusu vitu badala tu ya kujaribu kupitisha siku. Mungu atatupatia nguvu mpya na kutuwezesha kupambana na maisha bila kuchoka (tazama Isaya 40:31).
Sala ya Shukrani
Baba, ninashukuru kwamba unanipa amani na utulivu hata katikati ya siku ya shughuli nyingi. Nisaidie kukuegemea leo na kutumia hekima katika kupanga ratiba yangu. Wewe ni nguvu ya maisha yangu na ninakutegemea wewe kikamilifu.