Hekima katika Kungoja kwa Utulivu

Hekima katika Kungoja kwa Utulivu

Lakini Mariamu akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake. —LUKA 2:19

Kuna hekima kuu katika kujifunza kufikiri kimyakimya unachohisi Bwana amenena nawe, haswa usipojua kikamilifu vile kitakavyotendeka.

Huenda ukahisi Mungu ameahidi kitu kwa sababu ya wanao, amenena mwelekeo mpya kuhusu kazi yako, amekuagiza kufanya mabadiliko katika hulka yako—lolote lile, iwapo utamtumainia Mungu, ngoja kwa uvumilivu, na ufikirie kile Mungu amenena, atakuonyesha kabisa vile utakavyoshirikiana na mpango wake.

Mariamu alikuwa na vitu vizuri vya ajabu vilivyofanyika katika maisha yake. Alikuwa tu msichana mpevu aliyempenda Mungu malaika wa Bwana alipomtokea na kumwambia atakuwa mama ya Mwanawe Mungu. Lakini chochote kile Mary alifikiria au kuhisi, alimtumainia Mungu akisema, “Na iwe kwangu kama ulivyosema”(Luka 1:38).

Mungu anapotunenea kitu, mara nyingi tunahitaji kukinyamazia. Anapotuambia vitu ambavyo kwa kweli hatuelewi, vitu vinavyoonekana kukosa maana, tunaweza kufuata mfano wa Mariamu. Tunaweza kufikiria zaidi badala ya kukimbilia wengine kwa ushauri. Shaka la wengine linaweza kuharibu imani yako. Wakati mwingine kitu kizuri unachoweza kufanya ni kushikilia imani ahadi ya Mungu kwa utulivu na kumwambia akueleze dhahiri katika wakati wake mtimilifu.


Mungu anapokuita kufanya kitu, hukupa pia imani ya kukifanya.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon