Hukumu au Uhakikisho

Hukumu au Uhakikisho

Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. YOHANA 3:17

Kuna tofauti muhimu kati ya hukumu (hatia) na uhakikisho wa kweli kutoka kwa Mungu.

Hukumu hudhihirika kama mzigo mzito ambao hutuhitaji kulipia makosa na kasoro zetu na kutusukuma chini. Uhakikisho ni kazi ya Roho Mtakatifu, ambaye anatuonyesha kwamba tumetenda dhambi na kutualika kukiri dhambi zetu, kupokea msamaha na usaidizi wa Mungu kuboresha tabia zetu katika siku zijazo. Hukumu hufanya makosa yenyewe yaonekana mabaya zaidi; uhakikisho hukusudiwa kutuinua kutoka kwa makosa yenyewe.

Ukihisi uhakikisho, mshukuru tu Mungu kwa kuongea nawe, kiri dhambi yako kwake, na ugeuke kutoka kwa dhambi hiyo. Halafu… upokee Msamaha wa Mungu na kusahau dhambi hiyo! Mungu husamehe na kusahau, na ukitaka kuwa na furaha ya ukombozi ambao Mungu anataka sisi wote tuwe nao, utahitaji kuisahau pia.


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwamba hakuna hukumu ndani ya Yesu Kristo. Unaponihakikishia kwamba nimetenda dhambi, nisaidie kukuletea kwa toba bila kuhisi kwamba nimebebeshwa mzigo wa hatia na hukumu. Umenisamehe kwa hivyo leo ninachagua kujisamehe pia.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon