Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani, vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu. 1 WAKORINTHO 14:33 BIBLIA
Kuchanganyikiwa hakutoki kwa Mungu. Tunapochanganyikiwa, ni kwa sababu tunajaribu kwa bidii kufikiria vitu kwa kutegemea mawazo yetu badala ya kumwamini Mungu. Anatupatia amani, sio kuchanganyikiwa. Ukihisi kuchanganyikiwa, unafaa kutambua kwamba kuna kitu kisicho sawa kuhusu mtazamo wako wa maisha. Pengine umetoka kwa neema hadi kwa kazi zako. Hilo lina maana kuwa huenda ikawa unajaribu kusuluhisha shida zako badala ya kumtegemea Mungu. Lakini shukuru kuwa, unaweza kusalimisha bidii zako na ujisalimishe kabisa kwa Bwana, huku ukiachilia hali yako yote mikononi mwake.
Mara tu utakapogeuka na kutoka kwa bidii zako na kufikiri kwako hadi kwenye neema ya Mungu, utafungua mkondo wa imani ambapo ataanza kukufunulia unachohitaji kujua ili kukabiliana na shida au hali hiyo. Ingia kwenye raha ya Mungu, halafu utapata uongozi unaohitaji.
Sala ya Shukrani
Ninashukuru, Baba, kwamba unanipa amani badala ya kuchanganyikiwa. Nitaishi katika neema zako, nikijua kwamba unaweza kushughulikia hali yoyote ile ambayo huenda ikanikumba. Asante kwa amani yako—ninaipokea leo.