Mahusiano Huru Kutokana na Mfadhaiko

Mahusiano Huru Kutokana na Mfadhaiko

Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi. WAEFESO 4:32

Je, kuna mahusiano ambayo ni huru kabisa kutokana na mfadhaiko? Sina hakika, lakini shukuru kuwa kuna hatua ambazo tunaweza kuchukua ili kuboresha mahusiano yetu. Acha nipitie hatua nne nawe:

  • Hatua ya 1: Anzisha na udumishe amani nawe na amani na Mungu. Basi tu ndivyo utaweza kuanza kuwa na nia itakayokuwezesha kuishi na wengine.
  • Hatua ya 2: Usitarajie watu kuwa watimilifu, kwa sababu hawatawahi kuwa. Haya ni matarajio yasiyowezekana kwa sababu yataharibu mahusiano yako.
  • Hatua ya 3: Usitarajie kila mtu kuwa kama wewe kwa sababu hawako kama wewe. Unapogundua kuwa kila mmoja wetu ana tofauti za kipekee, itasaidia kusuluhisha migongano mingi,.
  • Hatua ya 4: Kuwa mhimizaji sio mkatisha tamaa. Kila mtu anapenda kuwa na watu ambao husherehekea na kutambua nguvu na kuchagua kupuuza udhaifu.

Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwa mahusiano niliyo nayo na watu walio katika maisha yangu. Acha upendo wako umininike kupitia kwangu ninapokusudia kuimarisha mahusiano haya. Ninakushukuru kwamba ninaweza kufanya jukumu langu la kujenga mahusiano yaliyo huru kutokana na mfadhaiko, yanayotoa uzima na yenye afya.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon