Huwezi Kuwa Peke Yako

Huwezi Kuwa Peke Yako

…Na tazama mimi nipo pamoja nanyi; siku zote, hata ukamilifu wa dahari. —MATHAYO 28:20

Mungu anataka ujue kwamba huwezi kuwa peke yako. Shetani atajaribu kukufanya uamini uko peke yako, lakini huo ni uongo. Atajaribu kukudanganya kwa kukuambia kwamba hakuna anayeelewa vile unavyohisi, lakini huo si ukweli. Licha ya Mungu kuwa nawe, waaminio wengi wanajua vile unavyohisi, na wanaelewa kile ambacho huenda unapitia.

Unapomfuata Mungu na kuendelea kupiga hatua ya kiroho, Shetani huleta mateso mara kwa mara ili akukatishe tamaa na kukufanya uhisi uko peke yako. Ninakumbuka wakati mmoja miaka mingi iliyopita, Mungu aliponiita kufanya jambo jipya na lilinihitaji kujitenga na watu wengi na vitu vingi ambavyo nilivipenda sana.

Mara nyingi lazima tuachilie vitu na mienendo ya zamani na ili tuchukue vipya ambavyo Mungu anavyo kwa ajili yetu. Nilikuwa mpweke mara kwa mara nilipokuwa nikijaribu kujenga maisha yangu mapya, lakini Mungu alikuwa nami katika kila hatua.

Iwapo unang’ang’ana na upweke pamoja na uchungu, toa nguvu kwa Mungu. Jua kwamba yuko nawe, na atakusongeza mbele. Ana uweza wa kubadilisha maombolezo yako yakawa furaha na kukufariji katika huzuni wako. Mwamini Mungu kwa moyo wako wote, na usiache Shetani aibe majaaliwa yako.


Tumainia upendo wa Mungu na ujue kwamba yuko nawe wakati wote.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon