Imani Kama ya Mtoto

Imani Kama ya Mtoto

. . . Basi yeyote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, [kuamini, mnyenyekevu, mwenye kupenda, kusamehe] huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni. —MATHAYO 18:4

Watoto huamini wanaloambiwa. Watu wengine husema watoto ni wadhaifu, lakini watoto si wadhaifu; ni wa kuamini. Ni kawaida ya mtoto kuamini isipokuwa kama amepitia hali iliyomfunza kinyume. Na kitu kingine ambacho sisi wote tunajua kuhusu watoto ni kwamba wanaweza kufurahia kitu chochote. Wanaweza hata kugeuza kazi kuwa mchezo!

Baba yetu wa mbinguni anatamani twende kwake kama watoto. Anataka tujue kwamba sisi ni tunu zake ndogo na tuweke imani yetu kikamilifu ndani yake kwamba atatutunza. Anataka tuushike mkono wake na tumwegemee, huku tukiomba usaidizi wake bila kukoma. Kila kitu ambacho Mungu anatuita kufanya, atatusaidia kukifanya. Yuko tayari, anangoja, na anataka sana. Tunaweza kuja kwa unyenyekevu kama watoto wadogo—kwa uaminifu, bila kujifanya, kwa ukweli na moyo uliofunguka—ukijua kwamba bila yeye, hatuwezi kufanya lolote.

Kama watoto wa Mungu, hatukukusudiwa kuishi katika utumwa wa namna yoyote. Tunaweza kuishi katika utukufu wa uhuru na haki—uhuru wa kufurahia kila kitu ambacho Mungu ametupatia ndani ya Kristo. Ametupatia uzima, na lengo letu liwe kuufurahia.


Tafuta kuwa, na kubaki kama mtoto na kuwa na urahisi wote wa maisha ya mtoto. Utaboresha kiwango cha maisha yako kwa njia ya ajabu mno.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon