Imani, Shukrani, na Utulivu

Imani, Shukrani, na Utulivu

Ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu bali katika nguvu za Mungu. 1 Wakorintho 2:5

Imani hutusaidia kutulia—kiakili na kihisia. Hata hiari yetu hutulia tunapokuwa na imani ndani ya Mungu. Hatuwi na wasiwasi wala kutegemea akili zetu, huwa hatufadhaiki wala kutaumauka, na hatujaribu kufanya kitu kisicholingana na mapenzi ya Mungu kufanyika—tunashukuru kwamba Mungu yuko mamlakani ili tupumzike!

Paulo alimwimbia Mungu sifa akiwa gerezani. Yesu aliwaombea wengine alipokuwa akisulubiwa. Yusufu aliamua kwamba iwapo atakuwa mtumwa, atakuwa mtumwa mzuri kabisa ambaye mtu aliyemmiliki hajawahi kuwa naye. Kote kwenye Maandiko, tunaona uhusiano kati ya imani, shukrani na utulivu.

Tunahitaji ukweli kuhusu kinachosababisha mfadhaiko wetu. Je, kweli ni hali zetu za maisha, au ni vile tunavyokabili hali zetu maishani? Kuna utulivu unaokuja na shukrani na imani. Huu ni utulivu ambao tunaweza kuishi nao kila siku.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru leo, Baba, kwamba ninaweza kuishi kwa utulivu. Sihitaji kuwa na wasiwasi au kutamauka ninapokabili changamoto. Asante kwa kuwa ninaweza kuwa na imani, nikijua kwamba ni wewe uko mamlakani.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon