Je, Nitakuwa na Vya Kutosha?

Kupanda Mbegu za Ushindi

Mkabidhi Bwana kazi yako, na mawazo yako yatathibitika. Mithali 16:3

Iwapo huna furaha na hali uliomo sasa hivi, je, utafanya bidii za kuibadilisha? Je, unataka kuwa katika hali hiyo hiyo wakati huu mwaka ujao? Au unataka kitu tofauti? Ukitaka kuwa na kitu tofauti, omba uongozi wa Bwana halafu uanze kwenda anavyokuelekeza. Unaweza kuchagua kulipa gharama upande huu ili uwe na kile unachotaka baadaye.

Itabidi utumie baadhi ya mwaka huu kusonga hadi kwenye malengo yako ya mwaka ujao. Unaposonga mbele, utahitaji kufanya maamuzi magumu, na utakuja kwenye njia panda zinazoumiza moyo. Lakini utakapofika mahali hapa, chuchumilia hadi mbele. Ukichuchumilia hadi mbele, unaweza kushukuru kwamba Mungu yu nawe, ili kukusaidia na kukutia nguvu. Ukianza kufanya kazi ukielekea kwenye lengo lako sasa hivi, utakuwa na ushindi unaoutazamia baadaye.


Sala ya Shukrani

Baba, ninaomba kuwa unisaidie kuwa na nidhamu ya kutosha kila siku ili kusonga mbele kwenye malengo yangu. Ninakushukuru kwamba una mpango mzuri juu ya maisha yangu, na kama nitafanya sehemu yangu, utafanya sehemu yako wakati wote.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon