Je, Umeunganishwa?

Je, Umeunganishwa?

Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu ombeni mtakalo lolote nanyi mtatendewa. Yohana 15:7 Biblia

Imani ndiyo kiungo chetu kwenye neema na nguvu za Mungu. Fikiria kuhusu taa. Taa inaweza kutoa mwangaza tu ikiunganishwa na chanzo cha nguvu za umeme. Ikitolewa, haitafanya kazi, hata kama tutawasha na kuzima swichi mara ngapi.

Wakati mmoja nilikuwa katika chumba cha hoteli nikijaribu kuwasha taa, na kwa mfadhaiko, nikafikiria, kwani hizi hoteli hata haziweza kupeana taa zinazofanya kazi?! Halafu mtu kutoka idara ya huduma za kiufundi akaja kwenye chumba changu na kugundua kwamba taa hiyo haikuwa imeungwa na nguvu za umeme.

Acha nikuulize, “Je, umeacha kuungwa?” Je, umeruhusu hofu kuiba imani yako? Iwapo ndiyo, usiwe na wasiwasi kuhusu hilo. Amua tu sasa hivi kwamba utashukuru kwa nafasi mpya. Amua kwamba utakuwa na nia mpya, ile iliyojaa ujasiri, ushupavu na imani. “Jiunganishe na uache nuru yako iangaze.”


Sala ya Shukrani

Baba, nisaidie kujiunganisha na nguvu zako leo. Ninakushukuru kwa ajili ya imani ambayo umenipa ambayo inahitaji tu kuchochewa. Leo ninaamini ahadi zako na kusimama katika imani nikiwa tayari kuzishuhudia zikija kutimia katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon