Jifunze kuchukua maisha jinsi yanavyokuja

Jifunze kuchukua maisha jinsi yanavyokuja

Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake. Mathayo 6:34

Kama watu wengi, mimi hupinga mambo ambayo sipendi na siwezi kufanya kitu chochote kuhusu. Siku moja Bwana aliniambia, “Joyce, jifunze kuchukua maisha jinsi yanavyokuja.” Naamini hili ni somo kwetu sisi sote.

Kile alichokuwa akaniambia ni kwamba nilihitaji kuacha kupambana na mambo ambayo siwezi kufanya chochote kuyahusu.

Ikiwa tunasafiri mahali fulani na ghafla tujikute kwenye trafiki nzito kutokana na ajali au hali mbaya ya hewa, haitufaidi kamwe kulipinga. Ni wakati tu au uingiliaji wa Mungu usio wa kawaida utabadilisha hali hiyo. Kwa nini usitulie na ujaribu kutafuta njia ya kufurahia wakati huo?

Mungu ametuwezesha kushughulikia maisha kama yanavyokuja, ndiyo sababu anatuambia tuzingatie leo. Anajua kwamba ikiwa tunatumia wakati tukiwa na wasiwasi juu ya maswala zaidi ya udhibiti wetu, tutachoka na kuchanganyikiwa.

Huna haja ya kupoteza muda kujaribu kubadilisha na kudhibiti vitu vilivyo nje ya udhibiti wako. Weka akili yako kufanya kile ambacho Mungu ameweka mbele yako na kumruhusu aangalie mengine.

 OMBI LA KUANZA SIKU

Bwana, natambua kwamba siwezi kudhibiti kila kitu, lakini ninaweza kukuamini. Hivi sasa, ninafanya uamuzi wa kufanya kazi nzuri na kile ulichonipa na kukuachia mengine

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon