Jiheshimu na Kujithamini

Jiheshimu na Kujithamini

Kwa maana ndugu mnaopendwa na Mungu, twajua uteule wenu. 1 Wathesalonike 1:4 Biblia

Yale tunayojitendea ndiyo tunayowatendea wengine. Hii ndiyo sababu moja ambayo tunahitaji kujipenda, bila kuwa wabinafsi.

Usifikirie kuhusu makosa yako. Sisi wote tuna nguvu na udhaifu. Tunafaa kutumia nguvu zetu bila kufadhaika kwa ajili ya udhaifu wetu, tukitambua kuwa nguvu za Mungu hutimilika katika udhaifu wetu (tazama 2 Wakorintho 12:9). Hata hivyo, tusingekuwa na udhaifu, tusingemhitaji Yesu. Alikuja kwa ajili ya wale wasiokuwa watimilifu na wadhaifu, na hao ni sisi wote.

Unaweza kufurahia kuwa na amani na nafsi yako, lakini itabidi uifuatilie. Fanya uamuzi kwamba, kwa sababu uko na nafsi yako wakati wote, unafaa kujipenda. Mungu alikuumba, na haumbi takataka, kwa hivyo anza kushukuru kwa uzuri wako na uache kufadhaika juu ya udhaifu wako.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru leo, Baba, kwamba unanipenda; umenichagua na kuniumba kama mtu mrembo wa kipekee. Nisaidie kujiona vile unavyoniona. Asante kwa kuwa ninaweza kuishi kwa amani, nikijua kwamba nimeumbwa nawe kwa jinsi ya ajabu ya kutisha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon