Jikabidhi kwa Mungu Halafu Utulie

Bwana Mungu wako yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa; atakushangilia kwa furaha kuu, atakutuliza katika upendo wake, atakufuarhia kwa kuimba (Sefania 3:17)

Ninaamini mojawapo ya shida kubwa inayowakabili watu leo ni mienendo yao ya maisha iliyo na shughuli nyingi, ya pupa, yenye mahangaiko na mifadhaiko. Kuwa na shughuli nyingi hufanya kusikia kutoka kwa Mungu kuwe na changamoto, lakini andiko la leo linaahidi kwamba Mungu atatutuliza katika upendo wake. Mojawapo ya hisani unayoweza kujifanyia ni kupata mahali unapoweza kutulia na kukimya.

Ili kusikia Mungu unahitaji wakati wa utulivu wa nafsi. Iwapo kweli unataka kusikia sauti yake tulivu ndogo, itabidi utulie. Unahitaji kwenda mahali na kuwa peke yako naye. Yesu alisema, “Ingia katika chumba chako cha ndani na ufunge mlango (Mathayo 6:6).

Dakika tu chache za amani na utulivu hazitafanya kazi kila wakati; unahitaji pia muda mrefu wenye kimya kumtafuta Mungu. Ni muhimu kuweza kutumia wako ukiwa na Mungu mbali na shughuli na panda shuka za maisha.

Unapokuwa peke yako na Mungu, usiwaze kuhusu matatizo yako. Mwombe hekima na nguvu zake. Mwombe uvuvio na uhuisho. Mwambie unataka kujua alicho nacho kuhusu maisha yako.

Mwambie akuambie anachotaka ufanye.

Mwambie akuambie asichotaka ufanye.

Jikabidhi kwa Mungu na usikilize. Unamheshimu kwa kumwendea. Utapata jibu kutoka kwake. Usipomsikia akizungumza wakati utakapokuwa na muda peke yako naye, isikujalishe. Umetimiza sehemu yako kwa kumtafuta na atakuelekeza maishani.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO: Ikiwa una shughuli nyingi sana kiasi cha kukosa muda na Mungu, basi bila shaka unashughulika sana!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon