Jinsi ya kudumu katika uwepo wake kila siku

Jinsi ya kudumu katika uwepo wake kila siku

Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.  Yohana 14:23

Maisha yetu yana shughuli nyingi na vizuizi vingi.Ni rahisi sana kushikika katika shughuli, wasiwasi na majukumu hadi tukasahau kile kilicho cha muhimu zaidi.

Kuna hadithi fupi ya kupendeza mwishoni mwa Luka 2 wakati Maria na Yusufu walimpeleka Yesu Yerusalemu kwa pasaka akiwa umri wa miaka 12. Baada ya sherehe walianza safari kurudi nyumbani wakidhani kwamba yuko nao.

Nami najiuliza, ni mara ngapi tunadhani Mungu yuko nasi ilhali tumeenenda katika shughuli zetu wenyewe.

Sasa jambo la kushangaza ni hili; Maria na Yusufu walikuwa wamesafiri siku nzima kutambua kuwa Yesu hakuwa nao na iliwachukua siku tatu kumpata. Siku tatu! Sasa ujumbe hapa ni huu; ni rahisi sana kwetu kuupoteza uwepo spesheli wa Mungu kuliko kuupata tena tunapoupoteza.

Inafaa tuwe waangalifu kusalia katika uwepo wa Mungu. Tunapofanya hivyo, Mungu hupata maskani mioyoni mwetu.

Hii huanza kwa kuwa watiifu kwa neno la Mungu. Njia moja ya kuonyesha ukomavu wa kiroho ni kuachana na tabia ambazo hazimpendezi Mungu, hii huonyesha kwamba unayajali yale anayofikiria.

Hii inamaanisha unakuwa mkarimu kwa watu, unajifundisha kusamehe, unaachana na migogoro na unaishi kwa amani. Tunapojifunza kuwa makini na maneno yaetu, kumshukuru Mungu na kuwainua wengine, tutazidi kuwa katika uwepo wa Mungu siku nzima.


Ombi La Kuanza Siku

Baba, asante kwa kufanya moyo wangu makao yako. Ninahitaji uwepo wako leo. Nisaidie nikuheshimu kwa mawazo na maneno yangu, na kuwa wa Baraka kwa wale walio karibu name.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon