Jinsi ya Kupalilia Tunda la Roho

Jinsi ya Kupalilia Tunda la Roho

Tukiishi kwa Roho na tuenende kwa Roho. — WAGALATIA 5:25

Roho Mtakatifu akiishi ndani yetu, tuna kila kitu alicho nacho. Tunda lake liko ndani ya roho zetu. Mbegu imepandwa. Kadri tulivyo karibu na Mungu, ndivyo tunavyoruhusu zaidi mbegu ya tunda kumea na kukomaa ndani yetu kwa kuipalilia.

Tunaweza kupalilia matunda yote ya Roho kwa njia ya kimatendo—kwa kudhamiria kupenda, na kujidhibiti, la kwanza na la mwisho katika orodha. Matunda yote yanategemea upendo na kwa kweli ni aina ya upendo, lakini yanadhibitiwa na udhibiti wa kibinafsi.

Iwapo unamakinikia kukuza tunda la upendo, hautakuwa asiye na uvumilivu, au mwenye kukosa huruma kwa watu. Utakuwa mwema kwao, kuwasaidia na mwaminifu. Utaamua kuishi maisha yako kwa njia inayowabariki wengine, badala ya kutazama mahitaji yako kwanza. Haya ni matokeo ya upendo.

Ujidhibiti wa kibinafsi hutusaidia kufanya uteuzi mdogo mdogo mchana kutwa ili uwiane na tunda la Roho. Tukitumia huo uteuzi mdogo mdogo kuwiana na tunda la Roho, tutaanza kuwa na desturi nzuri zenye afya zinazompendeza Mungu. Ukiendelea kupalilia desturi hizi, utakuza tunda hadi uwe na maisha yasiyo ya kawaida katika Roho.


Tunda letu “linapofinywa,” na kupatikana tukiwa hatuko tayari, tunagundua iwapo tunda letu limekuzwa au halijakuzwa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon