Kabili Ukweli

Kabili Ukweli

. . . Nanyi mkikaa katika Neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kwelikweli, tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. —YOHANA 8:31–32

Mtu yeyote anayehitaji uponyaji wa kihisia na urejesho kutoka kwa madhara yaliyopita analazimika kujifunza kukabili ukweli. Hatuwezi kuwekwa huru huku tukikataa kukubali yaliyotukumba. Iwapo umedhurika, zungumza na Mungu kuhusu jambo hilo kwa uwazi kwa sababu anajali kuhusu kila kitu kinachokuhusu.

Mara nyingi watu ambao wamepitia mateso au misiba mingine katika maisha yao hujaribu kujifanya kwamba hawajapitia hali hizo. Tajriba za awali za kiwewe zinaweza kutufanya tuharibiwe kihisia na tuumizwe baadaye maishani kwa sababu tutaanza kuwa na fikra na mitazamo kujihusu, inayotokana na mambo tuliyoyapitia.

Kutokana na tajriba yangu binafsi, na pia kutokana na miaka yangu katika huduma kwa wengine, nimekuja kutambua kwamba sisi wanadamu ni hodari wa kujenga kuta na kuficha vitu katika kona za giza, huku tukijifanya havikuwahi kufanyika. Huwa tunafanya hivi kwa sababu huenda ikaonekana kuwa rahisi. Lakini kupuuza masuala kutatuweka katika utumwa; kuyakabili kwa usaidizi wa Mungu kutatuweka huru.

Ni jambo zuri sana kuwa katika uhusiano na Yesu, kwa sababu hatuwezi kumficha chochote. Hata hivyo, tayari anajua kila kitu kutuhusu. Tunaweza kuja kwake kila siku na kujua kwamba tunapendwa na kukubalika bila kujali tuliyoyapitia au vile tulivyokabiliana nayo.


Ingawa inaweza kuwa vigumu kukabili ukweli, Yesu anaahidi kuwa nasi na kutuweka huru.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon