Karama ya Imani

…mwingine imani katika Roho yeye yule… (1 WAKORINTHO 12:9)

Ninaamini kuna watu fulani ambao Mungu hupatia karama ya imani  kwa sababu ya matukio maalum kama vile safari hatari za kimisheni au hali iliyo na changamoto. Karama hii inapotumikishwa ndani ya watu, wanakuwa na uwezo wa kumwamini Mungu kwa utulivu kwa ajili ya kitu ambacho wengine watakiona kuwa kigumu. Wanakuwa na imani kamilifu kwa ajili ya kitu ambacho wengine watakatishwa tamaa au hata kuogopeshwa nacho.

Mtu anayetumika katika karama ya imani anafaa kuwa mwangalifu ili asije akafikiria kwamba wasiokuwa na karama hii hawana imani, kwa kuwa karama ya imani inapotumika ndani ya mtu, huwa Mungu anampa huyo mtu kiasi kisicho cha kawaida cha imani ili kuhakikisha kwamba kusudi lake limetimizwa. Anaweza kutumiwa na Mungu kuleta ujasiri na utulivu kwa wengine, lakini lazima asalie mnyenyekevu na mwingi wa shukrani kwa kile Mungu amempa. Warumi 12:3 inasema, “Kwa maana kwa neema kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.”

Wakati wote Mungu atatupatia imani tunayohitaji ili kukabiliana na kile tunachohitaji kukabiliana nacho. Hata hivyo, karama ya imani hufanya mtu awe na ujasiri usio wa kawaida. Mtu yeyote anayetumika nayo anafaa kuwa mhisivu kutambua kwamba ujasiri huu ni karama kutoka kwa Mungu na kumshukuru kwa sababu hiyo.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Kuwa mwingi wa shukrani kwa imani ambayo Mungu hukupa ili ufanye vitu vigumu.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon