Karama ya Ndimi

Mwingine aina za lugha….(Wakorintho 12:8,10)

Waaminio katika sehemu zingine za mwili wa Kristo wanajulikana kuwa wanatumika katika karama za Roho pengine sana kuliko wengine wa usuli mwingine wa kiroho. Baadhi ya vikundi vya makanisa hufundisha kuhusu ubatizo na karama za Roho kila mara na kuona karama zikitumikishwa kila mara, ilhali kanisa zingine hazifundishi kuhusu karama hizo wala hata kuamini kwamba Wakristo wanaweza kuzipata leo. Karama hizi ni sehemu ya Maandiko na zinafaa kusomwa na kutafutwa na waaminio Yesu Kristo wote.

Kuzungumza kwa ndimi ni kuzungumza kwa lugha ya kiroho, moja ambayo Mungu huelewa lakini mzungumzaji na wengineo huenda wasiielewe. Ni muhimu kwa maombi ya kibinafsi na ushirika na Mungu nan i ya manufaa katika miktadha ya ushirika, lakini lazima iambatane na karama ya kiroho ya kufasiri (soma 1 Wakorintho 14:2, 27-28).

Huenda kupuuza karama za kiroho kukafunga milango kwa uvukaji mipaka na matumizi mabaya ya karama hizo ambayo hufanyika wakati mwingine, lakini pia hufunga mlango wa baraka zisizohesabika ambazo watu wanahitaji kuliko kitu kingine chochote katika maisha yao ya kila siku.

Lazima niseme vile Paulo alisema katika 1 Wakorintho 14:18 kwamba, Namshukuru Mungu ya kuwa nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote kwa sababu huniimarisha kiroho; huzidisha undani wangu na Mungu; na huniwezesha kusikia sauti yake kwa uwazi zaidi.

Ni wazi kuwa, Paulo alizungumza katika ndimi. Wanafunzi 120 waliojazwa na Roho Mtakatifu katika siku ya Pentekoste wote walizungumza kwa ndimi zingine. Waaminio wengine waliopokea ubatizo wa Roho Mtakatifu vile ilivyorekodiwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume waliongea katika ndimi. Kwa nini mimi na wewe tusitumike katika karama hii ya Roho?

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Jifungue kwa karama za Roho Mtakatifu na usiwahi kuwa na nia iliyofungika kwa kujifunza vitu vipya.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon