Karibu na Mungu katika Maombi

Karibu na Mungu katika Maombi

Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi lakini mwili ni dhaifu. —MATHAYO 26:41

Maombi ni silaha ya kiroho ambayo Mungu ametupatia kupigana vita. Maombi ni uhusiano na Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Ni kuja na kuomba usaidizi au kuzungumza na Mungu kuhusu kitu ambacho kinatukera. Maombi hukatiza mipango ya shetani ya uovu!

Ukitaka maisha ya maombi yenye matokeo, anzisha uhusiano mzuri wa kibinafsi na Baba. Jua kwamba anakupenda, kwamba ni mwingi wa huruma, kwamba atakusaidia. Pata kumjua Yesu. Ni rafiki yako. Alikufia. Pata kumjua Roho Mtakatifu. Huwa nawe kila wakati kama msaidizi wako. Mwache akusaidie.

Aina zote za maombi zinafaa kutumika katika safari yetu na Mungu. Kuna maombi ya makubaliano kati ya watu wawili na maombi ya umoja ya kikundi cha watu.

Kuna maombi ya shukrani, sifa na ibada, lalama, kuombea wengine, kujikabidhi kwake, na kujitenga. Katika maombi yoyote unayoyaleta mbele zake, jifunze kujaza Neno la Mungu katka maombi yako na uombe na hakikisho kwamba Mungu hutimiza Neno lake.


Huwa tunaelekea kuzima maombi, lakini ninapendekeza kwamba uombe moja kwa moja wakati wowote unapoona au kufikiria kuhusu hitaji!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon