Kesha na Kuomba

Kesha na Kuomba

Kesheni mwombe msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu. —MATHAYO 26:41

Hofu ni njia ya shetani ya kujaribu kutuzuia kwenda mbele ili tusifurahie maisha ambayo Yesu alikufa kutupatia. Na hofu humshambulia kila mtu wakati mwingine. Lakini hofu sio ukweli. Hofu ni ithibati za udanganyifu zinazoonekana kuwa za kweli.

Hofu ni uwezo unaoweza kudhoofisha maisha yetu tukiikubali, lakini Mungu anatamani kututia nguvu tunapokuwa na ushirika naye katika maombi. Imani huachiliwa kupitia kwa maombi, jambo ambalo hufanya nguvu kuu ziachiliwe kwa ajili ya maisha yetu.

Biblia inatufundisha “kukesha na kuomba.” Kwa usaidizi wa Mungu, tunaweza kujiangalia pamoja na hali zinazotuzunguka na kuwa macho kwa mashambulizi ambayo adui ataanzisha dhidi ya nia na hisia zetu. Mashambulizi haya yanapogunduliwa, tunaweza kwenda kwa Bwana mara moja katika maombi. Ni ngome yetu yenye nguvu, na tukiwa ndani yake hakuna cha kuogopa.

Njia nzuri ya kumpinga shetani ni kuomba. Maombi yetu ya uaminifu na ukweli yatatuleta karibu na Mungu. Na kadri tulivyo karibu na Mungu ndivyo inavyokuwa rahisi kuushinda woga.


Omba kuhusu kila kitu na usiogope chochote. Hofu ikibisha mlangoni, acha imani ijibu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon