Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. —2 TIMOTHEO 1:7
Sisi wote tumepewa masaa ishirini na manne kwa siku. Ni muhimu jimsi tunavyotumia wakati huo—vile tunavyodhibiti maeneo tofauti ya maisha yetu ili kuyatazama ifaavyo. Tunapokuwa na kazi nyingi bila kupumzika vizuri, tunatoka nje ya kiasi. Tunakuwa wafanyi kazi sugu na kuishia kuchoka na kudhoofika.
Mimi hupata ridhaa nyingi kutokana na utimilishaji kitu na kazi. Sipendi muda mwingi ulioharibiwa na shughuli zisizokuwa na maana. Lakini kwa kawaida, ni rahisi kwangu kutokuwa na kiasi katika eneo la kazi. Inanilazimu kuamua kwamba sitafanya kazi bali nitapumzika pia. Lazima liwe jambo muhimu la kwanza kwangu ili niwe mwenye afya na kuwa karibu na Mungu.
Lakini pia inawezekana kuwa na kupumzika kwingi na kazi chache. Suleimani anasema kwamba kupitia “…kwa utepetevu wa mikono nyumba huvuja” (Mhubiri 10:18). Kwa maneno mengine, watu wasiofanya kazi vya kutosha huishia mashakani. Hela zao, maisha ya kiroho, mali, miili na kila kitu huteseka kwa sababu hawafanyi kazi inayohitajika kufanywa ili mambo yawe na utaratibu.
Mwombe Mungu akusaidie uwe na kiasi kiletacho afya na kinachofaa cha kazi na kupumzika. Chukua muda kukamilisha kazi zilizo mbele yako, lakini kuwa na uhakika wa kukamata nafasi za kuwa na amani na ufurahie kupumzika. Yote ni muhimu. Kiasi ndio ufunguo!
Omba Mungu akuonyeshe vile utakavyoleta kiasi katika maisha yako kutoka hatua moja hadi nyingine!