Kipaji cha Sasa Hivi

Kipaji cha Sasa Hivi

Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake. MATHAYO 6:34

Kuna upako (Upako na nguvu za Mungu) juu ya siku hii. Katika Yohana 8:58, Yesu alijiita “Mimi Ndiye.” Iwapo mimi na wewe kama wanafunzi wake, tutajaribu kuishi tukishikilia mambo ya kale au yajayo, tutapata maisha yakiwa magumu kwetu kwa sababu Yesu huishi sasa hivi kila wakati.

Yesu ametueleza dhahiri kwamba hatuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu kitu chochote. Kile tunachohitaji kufanya ni kumtafuta na kutafuta njia zake, na atatuongezea chochote tunachokihitaji, hata kiwe ni chakula au mavazi au makao au ukuaji wa kiroho (Mathayo 6:25–33). Hatuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu kesho. Badala yake, tunaweza kumakinikia leo na kumshukuru Mungu kwa baraka za leo..

Tulia na uangaze! Cheka zaidi na upunguze wasiwasi. Usiharibu leo kwa kuwa na wasiwasi kuhusu jana au kesho—huwezi kufanya chochote kuhusu yote mawili. Furahia leo kama bado unaweza kufurahia!


Sala ya Shukrani

Ninashukuru, Baba, kwa hii siku ambayo umenipa. Kwa usaidizi wako, nitaishi sasa hivi, sio katika siku zilizopita au zijazo. Ninakushukuru kwa ajili ya kile umenihifadhia leo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon